Tuesday, February 24, 2015

Habari picha ziara ya Balozi wa Nia Njema wa SOS Dar es salaam

 Balozi wa Nia Njema wa SOS  Tanzania - Rais Mstaafu wa awamu  ya tatu Alhaji Ally Hassan Mwinyi (Babu) akimbusu mtoto aliyempa maua mara baada ya kuingia kijijini
Balozi na Nia Njema wa SOS Tanzania , Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya SOS Tanzania Dr. Mary Nagu (kulia) na Mkurugenzi wa Kijiji cha SOS Dar es salaam Dr. Alex Lengeju (kushoto) wakati wa ziara  ya Balozi huyo kijijini hapo

Babu (Mzee Mwinyi) alipata fursa ya kucheza kiduku na watoto wakati wa ziara yake

Babu akishuhudia maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa  na watoto wa kijiji 

 Mzee Mwinyi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa SOS  Tanzania  Rita Kaurananga wakati wa ziara yake 

Mwenyekiti wa Wadhamini wa Bodi ya SOS Tanzania Dr. Mary Nagu akimkabidhi tuzo Mzee Mwinyi kama ishara ya  Shukrani kwa kukubali kwake kuwa Balozi wa Nia Njema kwa SOS Tanzania

 Mzee Mwinyi alipata fursa ya kupiga  picha na baadhi ya Wafanyakazi wa Kijiji cha SOS  Dar Es Salaam na baadhi ya Wadhamini wa Bodi

 Hapa  akiwa na Baadhi ya Walezi wa watoto 

Mzee Mwinyi na baadhi ya Wadhamini wa Bodi ya SOS Tanzania

No comments:

Post a Comment